- Admin
- #1
Jinsi ya Kujisajili Kimtandao NIDA Mwombaji wa Utambulisho wa Taifa anatakiwa awe, raia au mgeni mkaazi anayeishi nchini kihalali na mwenye umri wa miaka 18 na zaidi.
Hatua za Kujisajili NIDA, Kimtandao:
i. Fungua kiunganishi wezeshi https://eonline.nida.go.tz kwa kutumia kifaa kilichounganishwa na mtandao (simu janja, kompyuta, laptop au tablet),
ii. Fungua akaunti kwa kutumia barua pepe yako, kisha thibitisha ujumbe utakaotumwa kwenye barua pepe hiyo. Hakikisha neno la siri lina herufi ndogo, kubwa, tarakimu pamoja na alama maalum na zote kwa ujumla wake zisiwe chini ya sita,
iii. Soma maelezo yote ya awali kwenye ukurasa wa mwanzo kabla ya kuanza kujisajili,
iv. Chagua fomu sahihi kulingana na hadhi ya uraia wako (1A kwa raia na 2A kwa mgeni mkaazi),
v. Taarifa za majina na mwaka wa kuzaliwa ziendane na nyaraka zako nyingine unazoziambatisha,
vi. Ambatisha nakala zako kama Cheti cha kuzaliwa, Cheti cha kidato cha nne (Leaving Certificate) barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji/Shehia, na kitambulisho cha mzazi walau mmoja/au au cheti chake cha kuzaliwa. Iwapo wote wanavyo ni vyema zaidi kuambatisha vyote,
vii. Chapisha fomu ya maombi pamoja na viambatisho. Kama kuna viambatisho visivyoweza kupakiwa mtandaoni, viambatisho kwa nakala ngumu baada ya kuchapisha,
viii. Peleka fomu kwenye Serikali ya Mtaa/Kijiji/Shehia ili igongwe muhuri (kipengele Na. 60) na kupata barua ya utambulisho wa makazi,
ix. Wasilisha fomu na viambatisho vyote ofisi ya NIDA ya wilaya yako kwa ajili ya kuchukuliwa picha, alama za vidole na saini ili kukamilisha usajili.
Mavazi ya kuzingatia wakati wa Usajili:
x. Ili picha ya mwombaji wa Utambulisho wa Taifa itoke katika ubora uliokusudiwa pindi unapopigwa picha wakati unapowasilisha fomu za maombi kwenye Ofisi ya Usajili ya NIDA katika wilaya unakoishi na kuchukuliwa alama za kibaiolojia (picha, alama za vidole na saini); epuka kuvaa kaptura, suruali au nguo za kubana, t-shirt, jeans, nguo zenye nembo/michoro, mavazi ya manguozi, kofia aina yoyote na kutopaka hina mikononi au usoni na kucha zisiwe zimepakwa rangi.
xi. Huduma ya Usajili hadi kupata Vitambulisho ni Bure kwa raia, Epuka Matapeli!
Kwa maelezo zaidi tafadhali fika kwenye Ofisi ya Usajili ya NIDA Wilayani au wasiliana na NIDA kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja kwa Namba: 0232210500, Tovuti www.nida.go.tz, Barua pepe info@nida.go.tz
Mitandao ya Kijamii:- Facebook, Instagram na X Nidatanzania.