Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Ofisi ya Rais - TAMISEMI) inasimamia utekelezaji wa Sera mbalimbali za Kisekta na Sheria ya Tawala za Mikoa Sura 97, Sheria ya Serikali za Mitaa Mamlaka za Wilaya, Sura 287, Sheria ya Serikali za Mitaa Mamlaka za Miji Sura 288 na Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Sura 448. Ofisi ya Rais-TAMISEMI inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidentrial Instrument) Namba. 144 ya tarehe 22 Aprili, 2016. Kimuundo Ofisi ya Rais-TAMISEMI ina Idara Tisa (9), Vitengo nane (8) na Taasisi Saba (7). Aidha, Ofisi ya Rais TAMISEMI inasimamia utekelezaji wa majukumu katika Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184 ambazo kati yake Halmashauri za Majiji ni 6, Halmashauri za Manispaa 20, Halmashauri za Miji 21 na Halmashauri za Wilaya 137, Mamlaka za Miji Midogo 71, Tarafa 570, Kata 3,956, Mitaa 4,263, Vijiji 12,318 na Vitongoji 64,384 hii ni mpaka 2020.
www.tamisemi.go.tz