Majukumu na kazi za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zinatokana na majukumu yake. Zifuatazo ni kazi na majukumu ya Ofisi ya Rais TAMISEMI:-
www.tamisemi.go.tz
- Kuzijengea uwezo wa Tawala za Mikoa, Kuratibu na Kufuatilia masuala ya Mikoa na msaada wa kiufundi unaotolewa na Sekretarieti za Mikoa kwa Halmashauri;
- Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa huduma bora;
- Kuratibu usimamizi wa jumla na usimamizi wa elimu ya awali, msingi, sekondari, mahitaji maalum, elimu ya watu wazima na elimu isiyo rasmi;
- Kuhakikisha maeneo ya vijijini na mijini yamepangwa ipasavyo yakiwa na maendeleo salama na endelevu katika nyanja za kiuchumi, kijamii, kimazingira na kisiasa;
- Kuratibu, kusaidia na kuwezesha matengenezo na maendeleo ya miundombinu ya barabara ndani ya Halmashauri;
- Kuratibu maingiliano muhimu ya OR-TAMISEMI na Wizara mama na Wizara za Sekta, Idara na Wakala, Watendaji wasio wa Serikali (Non State Actors), Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kuwezesha Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri kutoa taarifa na huduma bora na kwa wakati kupitia mifumo ya TEHAMA;
- Kufanya ukaguzi wa kawaida, haki na ufanisi na ufuatiliaji wa fedha zinazotumwa kwenda kwenye Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kutoa utaalamu na huduma katika kuboresha Mifumo ya Usimamizi na Miundo ya Shirika kwa ufanisi na ili kutoa huduma bora kwenye Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Taasisi zilizo chini ya OR-TAMISEMI;
- Kutoa mfumo wa huduma za kisheria kwa Mikoa na Halmashauri kwa ajili ya kukuza na kuendeleza Serikali za Mitaa;
- Kutoa usaidizi, mwongozo, uratibu, ufuatiliaji, juu ya kuwezesha usambazaji na utoaji wa usawa wa Huduma za Afya na Maendeleo ya Sekta ya Afya ndani ya Mikoa na Halmashauri;
- Kutoa utaalamu na huduma katika usimamizi wa rasilimali watu na masuala ya utawala kwa OR-TAMISEMI;
- Kutoa utaalamu na huduma katika uundaji wa sera, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini na mapitio yanayohusiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI;
- Kutoa usimamizi mzuri wa mifumo ya udhibiti na usimamizi wa fedha kwa OR-TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Taasisi zilizo chini ya OR-TAMISEMI;
- Kutoa utaalamu na huduma katika masuala ya ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa na huduma;
- Kutoa utaalamu na huduma katika masuala ya habari, mawasiliano na midahalo ya Umma na vyombo vya habari;
- Kuwezesha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Chaguzi za Ndogo) na;
- Kusimamia kazi za Taasisi zilizo chini yake.