VIPAUMBELE VYA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA TAMISEMI

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.

Cocoa

Administrator
Staff member
  1. Kusimamia shughuli za Utawala Bora, kukuza demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi na Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
  2. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za utoaji wa ElimuMsingi na Sekondari katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ikijumuisha utekelezaji wa ElimuMsingi na Sekondari Bila Ada;
  3. Kuratibu na kusimamia Mkakati wa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
  4. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za utoaji wa Huduma za Afya ya Msingi, Ustawi wa Jamii na Lishe katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
  5. Kushughulikia malalamiko ya walimu ikiwemo kutopandishwa vyeo kwa wakati; na wastaafu kucheleweshewa kulipwa stahiki na mafao yao baada ya kustaafu na kero zinazowakabili walimu waliostaafu;
  6. Kuchochea na kuhimiza ukuaji wa uchumi shindani kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla kwa kuiwezesha Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji, hasa katika Kilimo, Mifugo na Viwanda. Utekelezaji wa jambo hili umehusisha uimarishaji wa Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji na Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika ngazi ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuhakikisha kuna rasilimali watu wenye weledi pamoja na uwepo wa fedha na vitendea kazi;
  7. Kufanya Ukaguzi, Ufuatiliaji na Tathmini kuhusu utekelezaji wa shughuli za Taasisi, Programu na miradi katika ngazi ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
  8. Kusimamia mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika ngazi zote za Ofisi ya Rais - TAMISEMI;
  9. Kujenga uwezo wa watumishi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi;
  10. Kuratibu shughuli na utendaji kazi kwa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI;
  11. Kuratibu shughuli za ujenzi, matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya barabara, usafirishaji, maeneo ya utawala na maeneo ya kutolea huduma za jamii kwenye Taasisi, Mikoa, Wilaya na Halmashauri;
  12. Kusimamia matumizi ya rasilimali fedha katika ngazi zote za Ofisi ya Rais - TAMISEMI;
  13. Kuratibu uendelezaji wa Vijiji na Miji, na
  14. Kuratibu na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
 
Back
Top