- Admin
- #1
Majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania kwa mwaka 2025 yametangazwa rasmi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, vijana waliopata nafasi wanatakiwa kuripoti katika Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 30 Septemba 2024 hadi 2 Oktoba 2024 kwa ajili ya mafunzo. Kwa wale waliopitia usaili katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) na vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi, wanapaswa kuripoti Dar es Salaam katika eneo la Polisi (Barracks) Barabara ya Kilwa karibu na Hospitali Kuu ya Polisi mnamo tarehe 30 Septemba 2024 saa 12:00 asubuhi kwa ajili ya safari ya kuelekea Shule ya Polisi Moshi. Vijana waliopitia usaili katika mikoa ya Tanzania Bara wanapaswa kuripoti kwa makamanda wa polisi wa mikoa yao tarehe 29 Septemba 2024 saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
Kwa orodha kamili ya majina ya waliochaguliwa, unaweza kutembelea tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi Tanzania.
Kwa orodha kamili ya majina ya waliochaguliwa, unaweza kutembelea tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi Tanzania.