Majina ya waliochaguliwa Polisi

Cocoa

Administrator
Staff member
Reaction score
7
Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza majina ya vijana 3,500 waliochaguliwa kujiunga na jeshi hilo kwa mwaka 2024. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, vijana hawa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 30 Septemba hadi 2 Oktoba 2024 kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo. Vijana waliofanyiwa usaili katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) na vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam eneo la Polisi (Barracks) Barabara ya Kilwa karibu na Hospitali Kuu ya Polisi tarehe 30 Septemba 2024 kuanzia saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi. Kwa wale waliofanya usaili katika mikoa ya Tanzania Bara, wanatakiwa kuripoti kwa makamanda wa polisi wa mikoa yao tarehe 29 Septemba 2024 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.

Angalia majina hapa.
Majina ya waliochaguliwa Polisi
 
Back
Top