Ongezeko la kasi ya ujenzi ni moja ya sababu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa na uwezo mdogo wa kupanga, kusimamia na kudhibiti uendelezaji na hivyo kufanya usimamizi wa ukaguzi wa ujenzi wa majengo uwe dhaifu na majengo kuwa na viwango hafifu na kukosa usalama. Ukaguzi wa ujenzi wa majengo haufanyiki inavyotakiwa hivyo, kuathiri ubora wa majengo.
Waendelezaji wengi hawatumii ipasavyo ushauri wa kitaalamu na baadhi ya Makampuni yasiyozingatia maadili ya kitaaluma huonyesha majina na ushiriki wao kwenye mabango yenye taarifa za Ujenzi. Wapo pia, wataalam wanao saini kwenye vitabu vya ukaguzi (Inspection books) bila ya kukagua jengo husika kama inavyotakiwa.
Mwendelezaji anao mchango mkubwa katika kufikia ubora wa jengo uliokusudiwa. Vile vile, ni wajibu wake kuzingatia maelekezo yote yaliyomo kwenye Kibali cha Ujenzi kilichotolewa. Iwapo atamwaajiri mtaalamu mshauri na mkandarasi mahiri na mwaminifu,itarahisisha kazi ya ukaguzi. Kumekuwepo na udhaifu kwenye usimamizi unaosababishwa na waendelezaji kuajiri wataalamu washauri wasio na sifa na baadhi yao kutotembelea maeneo ya Ujenzi kufanya ukaguzi.
Hivyo, Ofisi ya Rais –TAMISEMI iliandaa Mwongozo utakaotumika wakati wa kutoa Vibali vya Ujenzi na Usimamizi wa Ukaguzi wa Ujenzi wa Majengo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Mwongozo huu umeandaliwa ili kuondoa changamoto zilizopo kwenye utaratibu wa utoaji wa Vibali vya Ujenzi na usimamizi wa Ujenzi wa majengo.
Kwa mujibu wa Vifungu 124 na 125 vya Kanuni za Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) (Udhibiti Uendelezaji), Sura 288 (GN 242 ya mwaka 2008), Ujenzi wowote ndani ya Mamlaka za Upangaji ambazo ni Mamlaka za Miji Midogo, Halmashauri za Miji, Manispaa na Ma-jiji ni lazima upate kibali cha Ujenzi kutoka kwenye Mamlaka husika.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 35 (i) cha Sheria ya Mipangomiji Na. 8 ya mwaka 2007, Mamlaka ya Upangaji inatakiwa kutoa kibali cha Ujenzi katika kipindi kisichozidi siku 60 kuanzia tarehe mwombaji alipowasilisha maombi yake. Aidha, ndani ya muda huo mamlaka inatakiwa kumjulisha mwombaji kuwa amekubaliwa au amekataliwa ombi lake na kutaja sababu zilizopelekea ombi lake kukataliwa.
Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Kifungu 122(4) imezipa majukumu Mamlaka za Wilaya ya kutoa au kubadilisha majina, namba za barabara, mitaa na nyumba kama ilivyobainishwa kwenye Mwongozo wa Anwani za Makazi na Postikodi wa Agosti 2016. Kufanya hivyo, kutadhibiti uendelezaji holela wa Vijiji na Miji Midogo inayochipukia.
Mwongozo huu ukifuatwa kikamilifu, kwa kigezo cha kiashiria cha utoaji wa Vibali vya Ujenzi, utaboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Mamlaka hizo zinatakiwa kutoa Vibali vya Ujenzi ndani ya kipindi cha kati ya siku saba na mwezi mmoja. Pia, mwongozo utaboresha usimamizi wa ukaguzi wa Ujenzi wa majengo.
Mwongozo wa Utoaji Vibali vya Ujenzi