Kwanini Anwani za Makazi?

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.

Cocoa

Administrator
Staff member
Majukumu ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ni pamoja na kupanga, kupima, kugawa, kumilikisha na kusimamia uendelezaji wa makazi katika maeneo ya utawala. Utaratibu huu unahitaji ufanisi katika usimamizi na udhibiti wa uendelezaji wa makazi na matumizi mengine. Utaratibu uliopo ni wa kutoa vibali vya kuendeleza maeneo yote yaliyopimwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa baada ya kuzingatia masuala muhimu ya uendelezaji kama vile umiliki, matumizi ya Ardhi, upimaji na masharti mengine ya uendelezaji.

Hata hivyo, kutokana na kasi kubwa ya ongezeko la watu na mahitaji makubwa ya makazi, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeshindwa kukidhi matakwa ya kupima maeneo ya kutosha ambayo wananchi wanaweza kuendeleza makazi yao kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Hali hii imefanya majengo mengi kujengwa bila vibali vya ujenzi na mengine kuendelezwa kwenye maeneo yasiyopimwa hivyo kuleta changamoto ya uundaji wa anwani za makazi. Itazingatiwa kuwa utaratibu wa anwani za makazi ulikuwepo siku za nyuma hususani miongo miwili baada ya uhuru na kufifia baadae kutokana na mabadiliko mbalimbali ya kiutawala na kisiasa.

Kutokuwepo kwa majina ya barabara, njia na nambari za nyumba ikichangiwa na ukuaji wa maeneo ya mijini, inaleta tatizo kwa sababu huduma nyingi za miji zinaathiriwa zikiwa ni pamoja na huduma za kijamii, kiuchumi na miundombinu. Ili kuondokana na matatizo yaliyoelezwa hapo juu, Wizara zenye dhamana na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa pande zote za Muungano, zilipewa jukumu la kutoa Mwongozo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini ili ziweze kutoa anwani za makazi kwa wananchi wote.

Mwongozo wa Anwani za Makazi
 
Back
Top