Maombi ya Marekebisho ya Majina kwenye Cheti NECTA

Cocoa

Administrator
Staff member
Reaction score
4
Maombi ya Marekebisho ya Majina kwenye Cheti NECTA - Baraza la Mitihani la Tanzania hushughulikia maombi ya marekebisho ya majina ya watahiniwa yaliyokosewa kuandikwa katika mitihani ya Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu. Ufuatao ni utaratibu unaotumika katika kuwasilisha maombi na kufanya marekebisho.

Maombi ya Marekebisho ya Majina kwenye Cheti NECTA

HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA KUFANYA MAOMBI
1. Fungua tovuti (Website) ya NECTA (necta.go.tz)
  • Chagua na ubonyeze huduma mtandao (E-services)
  • Ingiza Nambari ya simu ili kupata nambari ya uthibitisho (code number)
  • Ingiza nambari ya uthibitisho (Code) uliyopokea kwenye simu yako (tarakimu nne [04])
  • Ingiza barua pepe yako.
2. Namna ya kufanya malipo kwa kutumia ‘Control Number.
  • Ingiza majina ya mwombaji kama yalivyoandikwa kwenye cheti / Hati ya matokeo.
  • Ingiza tena nambari yako ya simu
  • Ingiza tena anwani yako ya barua pepe
  • Chagua huduma (Correction of Names)
  • Tengeneza control number (Generate Bill).
  • Lipia ada ya marekebisho ya jina ya Tsh.35, 000/= (kwa cheti kimoja) kupitia benki au mitandao ya simu kwa kutumia ‘Control number’ uliyotengeneza.
3. Baada ya kufanya malipo
  • Bonyeza Marekebisho ya Majina (Correction of Names) na ufanye maombi (Apply/New)
  • Ingiza nambari ya simu ya mkononi na nambari ya malipo (Control Number).
Jaza fomu ya maombi mtandao (Online Application Form) kisha Wasilisha ombi kwa kubofya ‘Submit’.

Baada ya marekebisho kufanyika, Hati ya Matokeo (Results Slip) au cheti kipya chenye marekebisho kitatumwa kwa mkuu wa shule au kwa mtahiniwa (endapo si mwanafunzi).
 
Back
Top